DINI ZA MZUNGU NA MWARABU (DINI ZA KUJA NA MELI)


- Hii sentence huwa na maana nyingi, Kiufupi tuseme, sentence hii humaanisha Imani ambazo tunaamini (Ukristu ama Uislamu) ni imani za Jamii fulani tu, Yaani wao ndio wakatuletea sisi, Yaani Ukristu labda ni Mali ya Mzungu? Kisha Uislamu ni Mali ya Muarabu?

- Hii nakataa! Sababu sina Imani kama Mzungu ndio Mwanzilishi wa Ukristu, Ama mzungu ndio Alipractise Ukristu toka zamani, Nina Hoja zangu ambazo siwezi sema kama ni Rasmi.

- Kwanza Mzungu mwenyewe hapo Mwanzo alikua Mpagani Kama Sisi Babu zetu walivyokua Wapagani, Kilichomfanya yeye aje Kutulete Ukristu ni Sababu yeye alikua jirani na walioushuhudia.

- Tuseme Kuhusu Swala La Imani, Ama Uwepo wa Mungu, Yawezekana Mzungu ndio alikua mjinga kama sisi Lakini alikua mwepesi Kuelewa Imani Mpya, Pia imani yake ya Kwanza Akaiita jina zuri na si jina la Upagani.

- Mfano Katika Wayunani (Wagiriki) na Warumi (Waroma), Jamii Mama za Ulaya, Jamii ambazo Ustaarabu wote wa Dunia yaani SIASA, MIFUMO YA ELIMU, UFUNDI, SAYANSI, SANAA nakadhalika vyote vimeanzia pale, Lakini Ukichukua Historia ya Imani ya Wagiriki na Warumi kabla hawajaujua Ukristu unaweza Ukacheka, Sababu ni Kama walikua wanaamini kitu cha ajabu sana.

Ukisoma Matendo 28:11 Kwa Kiswahili inasema:

"Baada ya miezi mitatu tukasafiri katika Merikebu ya Alexandria iliyokua imekaa pale Kisiwani wakati wa Baridi; na alama yake ni Ndugu Pacha"

- Mstari Huu Katika lugha ya Kiswahili hauleweki, labda Sijui kama wewe Umeuelewa !?, Hata kama Umeelewa basi umeelewa kitu ambacho hakijamaanishwa, Tukienda Katika Biblia za Kiingereza mstari huu unasema:

"After three months we put out to sea in a ship that had wintered in the island,it was an Alexandrian ship with the FIGUREHEAD of the twin gods CASTOR and POLLUX"

- Hapa Sasa unaweza Pata maana kwamba, Paulo Alipanda Merikebu ambayo Mbele ya Ile Merikebu kulikua na Alama ama Kielezo "Figurehead" sanamu ya "miungu mapacha.

- Figurehead ilikua ni kama sanamu ambayo ilikua ikiwekwa mbele kabisa ya Meli hapo zamani, Ilikua ni kama mapambo pia, Lakini mara nyingine ilikua ni sanamu ya "Role of Ship" yaani mfano Tanzania kuwe na Meli inaitwa MV Nyerere, Basi mbele ya Meli Kuwe na Sanamu ya Nyerere, Nadhani Umenipata......

- Sasa Paulo anasema kuwa ile meli ilikua na Sanamu ya miungu Mapacha ambao waliitwa CASTOR na POLLUX.

- Hawa Castor na Pollux ni miungu wa kale Wa Ugiriki, Pia Hata katika Rumi ya kale walijulikana kwa jina moja la DIOSCURI.

- Mama wa hawa CASTOR na POLLUX aliitwa Leda, Lakini walikua na Baba tofauti, Baba wa Castor aliitwa Tyndareus, Na Baba wa Pollux aliitwa ZEUS.

- Wagiriki Wa Kale Waliamini mungu mkuu (supreme deity) anaitwa Zeus na Waroma aliitwa Jupiter, Yaani Waliamini kuna miungu wengi (deities), ila mkuu wao ni mungu Zeus/Jupiter, Ambaye Pia Alijulikana kama "God Of thunder" sababu waliamini ndiye alikua akipiga Radi.

- Tumchunguze huyu Zeus Kiundani Kadiri ya Vitabu vya Greek Mythology ambaye ndie wanasema alikua mungu mkuu, kumbuka kwanza alikua na wazazi waliitwa mungu Kronos na Rhea.

Kronos (Baba wa Zeus) ndiye alikua mungu mkuu kabla, Sasa siku moja Kronos alipewa Unabii na mzazi wake aliyeitwa Gaia kwamba, Moja ya Watoto wake watakaozaliwa, lazima mmoja atampindua cheo chake kama yeye alivyompindua Baba yake huko nyuma.

- Kronos alipopata huu unabii aliamua kumeza Kila mtoto anayezaliwa na Wake zake, Aliogopa kupinduliwa kama yeye alivyompindua Baba yake aliyeitwa Uranus, Alimeza Jumla ya watoto watano.

- Mke wake aliyeitwa Rhea alipata ujauzito wa mtoto wake wa Sita, Wakati wa ujauzito kitendo cha Mumewe kumeza watoto kilimsababishia huzuni "unceasing grief" alipokaribia Kujifungua aliamua kuwaelekeza nia wazazi wake ya Kumsave mtoto wake kama kisasi (retribution) cha Kupinduliwa Babaye hivyo alisafiri mpaka mji ulioitwa Crete, Kisha Akajifungua huko na Kumuacha Mtoto kwa Mama wa Kronos, ambaye alimlea Mtoto huyo Katika Pango lililokua katika Mlima Aegaeon, Kisha Rhea akachukua Jiwe, akalifunga vitambaa na kumpelekea Kronos, Kronos Akameza bila hata Kuangalia ni Nini kilichomo.

Kitabu cha THE  SECRET TEACHINGS OF ALL AGES kilichoandikwa na Manly Palmer Hall kinasema Zeus alitunzwa Pangoni na Kukua kwa Haraka sana isivyo kawaida.

- Zeu akiwa kijana Alitumia mbinu na dawa kumlazimisha baba yake kutapika watoto wote aliowahi kumeza pamoja na Jiwe, Baadaye aliungana na wakubwa zake na pamoja walimshambulia Baba yao Kronos na kumshinda.

- Aliungana na miungu wenye vinasaba moja (Theogony) na Kupigana na miungu wa Sehemu nyingine vita hii iliitwa Gigantomachy na waliopigana Vita hii ni ndugu wa Zeus na the Olympians.

- ni story ndefu, lakini tuishie kwa Kusema Zeus alimwoa dadake Hera akazaa watoto naye lakini alitoroka mara kwa mara kufanya mapenzi na miungu wa kike wengine au na mabinti wa kibinadamu; mitholojia ya Wagiriki ilitaja zaidi ya majina 30 ya miungu au mabinti aliozaa nao.

- Ukitaka kujua Zaidi kupitia filamu, tafuta filamu inaitwa Jason and the Argonauts, au Tv Series inaitwa Hercules: The Legendary Journeys.

Haya mambo ya imani juu ya mungu Zeus ni ya miaka 700-730 Kabla ya Kristu, Lakini wagiriki waliamini Zeus ni mungu mkuu mpaka wakati wa Yesu Kristu na mpaka Wakati wa Mtume Paulo, Hawakuiacha imani yao.

Ukisoma Matendo 14:8-16 utaona Paulo na Barnaba walipokua mjini Listra ambayo ni Uturuki ya Leo, Walimponya kiwete, wenyeji wakaongea lugha yao ya asili (Lycaonian language) wakasema "miungu wametushukia kwa mifano ya wanadamu" Wakamwita Barnaba, Zeus, na Paulo wakamwita Hermes" huyu mungu Hermes alikua ni mtoto wa Zeus.

Katika mstari wa 13 anatajwa Kuhani wa Zeus, ambaye alikua tayari kutoa kafara ya mnyama "Ng'ombe" kwa kua aliamini miungu wao Wakipagani Zeus na Hermes wameshuka kwa njia ya binadamu "Paulo na Barnaba) mpaka Paulo Na Barnaba walipopata habari hii waliamua Kurarua nguo zao ili kuwaaminisha wao ni Binadamu sawa ba wengine, Na wakawahubiria Kuyaacha mambo yale ya Ubatili.

Kumbuka katika Historia, Paulo na Barnaba walienda Listra mwaka 48 Baada ya Kristu, Pi wakaenda tena mwaka 51 Baada ya Kristu, Hivyo kumbe Wazungu walikuwa wapagani toka Miaka ya 700 kabla ya Kristu, Mpaka Kristu anakufa aliwaacha wakiwa wapagani, akaja Paulo mpaka akararua nguo kuwaaminisha mwaka 48.

Polycarp Mdemu

Comments