WAKATI WA UCHAGUZI WA PAPA BENEDICT XVI

 



 WAKATI WA UCHAGUZI WA PAPA BENEDICT XVI makuu nje ya mkutano yalikuwa ni mawili. 

1. if not Ratzinger, who? (Kama sio Retzinger, Nani? 

2. why not Ratzinger? (Kwanini asiwe Retzinger?) 

Jarida la Time la tarehe  2 january 2005 lilinukuu vyanzo vya habari vya vatican ambavyo havikutajwa jina vikisema, Retzinger alikua moja ya warithi wa Papa john Paul II endapo angekufa au kudhoofika kimwili. hata jarida lilipopiga kura, alikosa kura moja tu kati ya nane, lakini yeye alisema anapenda kustaafu akiwa kijijini kwao akiandika vitabu.

Baada ya siku mbili za Conclave, Retzinger alichaguliwa baada ya kupigwa kura mara nne, Kabla ya Kura ya mara ya mwisho kuhesabiwa Kardinali Cormac Murphy-O'Connor alisema; 

"Ni jambo la kusikitisha sana mnapopanda mmoja baada ya mwingine kuweka kura yako kwenye chungu na unatazama juu kwenye picha ya Hukumu ya Mwisho ya Michelangelo. Na bado ninamkumbuka waziwazi kuwa aliyekuwa Kadinali Ratzinger ameketi kwenye ukingo wa kiti chake." 

Ni kweli Retzinger alishinda na kuchagua jina BENEDICT XIV ushindi wake ulitangwazwa kwenye Wimbi la waumini katika Basilica la Mtakatifu Petro.  aliyetangaza alikuwa ni Jorge Medina (Cardinal Protodeacon of the catholic church) Jorge Madina alipofika katika Balcony alitamka maneno "Dearest brothers and sisters" kwa lugha tano ( Kiitaliano, Kihispaniola, kifaransa, Kijerumani na Kiingereza) huku kila lugha ikipokewa kwa shangwe tangazo hilo, kisha Jorge madena akamalizia tangazo kwa lugha ya asili ya kanisa Kilatini kwa kusema "Habemus Papam" akiwa na maana "Tunaye Papa" baada ya hapo Papa mpya akajitokeza na kutoa Baraka maarufu inayoitwa  "Urbi et Orbi"

Maneno ya Kwanza kabisa ya Papa Benedicto kwa waumini alisema; "Ndugu wapendwa, baada ya Papa mkuu Yohane Paulo II, Makardinali wamenichagua mimi, mtenda kazi rahisi na mnyenyekevu katika shamba la mizabibu la Bwana. Ukweli ni kwamba Bwana anajua jinsi ya kufanya kazi na kutenda hata kama vifaa ni vichache......" 

(Hapa aliamini alipewa cheo kikubwa zaidi, kiufupi aliamini amepewa jukumu kubwa sana) akaendelea kwa kusema 

"....na zaidi ya yote ninajikabidhi kwa maombi yako. Katika furaha ya Bwana Mfufuka, tukiwa na uhakika wa msaada wake usioshindwa, tusonge mbele. Bwana atatusaidia, na Mariamu, Mama yake Mtakatifu zaidi, atakuwa upande wetu. Asante.

PAPA BENEDICT XIV alichaguliwa  kuwa Papa wa 265 katika orodha ya mapapa akiwa na miaka 78. hii ilimfanya kuwa Kardinali mwenye umri mkubwa zaidi kuchaguliwa kuwa Papa tangu papa clement aliyechaguliwa mwaka 1730 akiwa na miaka 78 pia.

Papa wa mwisho kuchagua jina BENEDICT  alikua ni Papa Benedict XV ambaye alikua ni muitaliano aliyeliongoza kanisa katika kipindi Kigumu cha vita ya kwanza ya Dunia, yeye aliingia madarakani mwaka 1914 ambapo vita ya kwanza ya dunia ilikua inaanza mwaka huo, vita ya dunia ikaisha mwaka 1918 na kumuacha akiwa madarakani kisha kufariki mwaka 1922, nadhani ndio maana hata Benedict XVI alichagua jina hili maana yeye pia alipigana vita ya pili ya dunia akiwa upande wa hitler.

Pope Benedict na Papa John Paul II ni mapapa waliofuatana wasiokua waitaliano, ni kitendo ambacho kilitokea miaka 600 nyuma wa kipindi kilichoitwa "avignon Papacy" kilichoanzia mwaka 1309 mpaka mwaka 1378, hivyo kwa miaka 600 mapapa walitoka nchini Italy kisha akafuata John Paul II.

Papa Benedict XVI Alipigana Vita ya Pili ya Dunia Akiwa Upande Wa Hitler, watu hili huona kama Papa alikua upande wa waovu, lakini ni hivi; Familia ya Mzee Ratzinger, hasa baba, ilichukia sana Wanazi, na upinzani wa baba yake dhidi ya Unazi ulifanya kushushwa cheo na kunyanyaswa kwa familia hiyo.

Ilipofika siku yake ya kumbukizi ya kuzaliwa mwaka 1941, Ratzinger aliandikishwa kujiunga na uanachama wa Hitler (Hitler Youth) hii ilikua ni sheria iliyopitishwa mwaka 1939 kwamba wavulana wote wa kijerumani wenye miaka kuanzia 14 lazima wajiunge.

kulingana na maelezo ya ndugu yake, Kijana Retzinger hakuwa na shauku na hakuwahi kuhudhuria mkutano wowote, mmoja wa binamu wa Papa Benedict aliyekuwa na miaka 14 alichukuliwa kipindi hicho hicho akiwa na ugonjwa wa Down Syndrome na kwenda kuuwawa wakati wa kampeni ActionT4

mwaka 1943 Retzinger akiwa bado mseminari aliandikiswa katika jeshi la ujerumani na kupambana katika kitengo cha Anti-Aircrafts, kujibu na kudungua mashambulizi ya anga, baadaye alifunzwa na kuwa askari wa ardhini (infantry) na aliporudi vitani alikamatwa na kufungwa katika kambi ya wafungwa wa kivita na kuachiliwa miezi kadhaa mwaka 1945.

Pia unatakiwa kujua, Papa Benedict xiv na kaka yake Georg Retzinger wote walichaguliwa kujiunga na Saint Michael Seminary mwaka 1945 baada ya kutoka ufungwani, pia wakaenda masomoni Chuo kikuu cha Ludwing Maxmilian huko Munich, na baadae wote wakapadrishwa mjini Freising tarehe 29-june-1951 na kardinali  Michael von Faulhaber.

Tunatakiwa Kujua Papa Benedict XIV aliweza Kuwa Professor akiwa na Miaka 31 tu mnamo mwaka 1958, Baada ya kuwa Professor wa teolojia katika vyuo kadhaa huko Ujerumani Papa Paul V mwaka 1977 alimteua kuwa Askofu Mkuu wa Majimbo ya Munich na Freising na kupewa Ukardinali, Ilishangaza kwakuwa Uteuzi ulitolewa kwa mtu mwenye uzoefu mdogo katika uchungaji (an unusual promotion for someone with little pastoral experience).

Anatajwa kama Moja ya Papa aliyeimarisha zaidi mahusiano ya Kanisa katoliki na sanaa (iconography), Pia kuhimiza Kanisa kurudi katika luhga yake ya Asili (latin), Pia kuanzisha upya mavazi maalumu ya Papa (Papal regalia and insignia) alitangaza vazi jipya maalumu kwa papa lililoitwa pallium hili liliwahi kuwepo zamani katika historia ya kanisa, linafanana na vazi lililoitwa  omophorion kwa wakristu wa mashariki, hii ilimfanya kupewa jina jipya "the pope of aesthetics" pia miaka ya 1980 alitajwa kama "the main intellectual force in the Church" yaani "Nguvu kuu ya kiakili katika kanisa"

Waandishi wengi husema alikuwa "sura kuu" (major figure) kwenye majukwaa ya vatican kwa robo nzima ya karne, Yaani niseme alikuwa na ushawishi zaidi, second to None linapokuja suala zima la kujadili ama kuweka vipaumbele vya kanisa ama mwelekeo, pia alikua mmoja ya wasiri wa karibu wa Papa John Paul II, Hii imemfanya kuishi Mjini Roma toka mwaka 1981 mpaka kufikwa na mauti mwaka huu 2022.

MUNGU AMLAZE MAHALA PEMA PEPONI. AMINA

Polycarp Mdemu

Comments